Hatimaye Afrika imepata uongozi wa Shirika la Biashara duniani (WTO), baada ya Ngozi Okonjo Iwela (66), raia wa Nigeria kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WTO, wadhfa ambao atauchukua rasmi kuanzia Machi mosi 2021.
Daktari Okonjo ambaye ni mama wa watoto wanne atakuwa mwanamke wa kwanza kuliongoza shirika hilo.
Katika kipindi cha miaka 25 alipokuwa akifanya kazi katika Benki ya Dunia, anatambuliwa kwa kuongoza miradi kadhaa kusaidia nchi zenye kipato cha chini, hasa kwa kukusanya karibu dola bilioni 50 mwaka 2010 kutoka kwa wafadhili wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA), mfuko wa Benki ya Dunia kwa ajili ya nchi maskini.
Lakini katika mabadiliko aliyoleta nchini Nigeria anayojivunia hasa -ni kuhudumu kama Waziri wa fedha mara mbili chini ya rais Olusegun Obasanjo na Goodluck Jonathan.