Viongozi wa vyama vya soka barani Afrika, wapendekeza nafasi 10 kwa ajili ya mataifa ya bara hilo kushiriki kwenye fainali za kombe la dunia, ambazo kuanzia mwaka 2026 zitashirikisha mataifa 48.

Pendekezo hilo kwa FIFA limetolewa na viongozi wa soka wa Afrika katika mkutano maalum ambao ulimshirikisha rais wa shirikisho hilo la soka duniani.

Rais wa chama cha soka Afrika kusini Daniel Alexander “Danny” Jordaan aliwaambia waandishi wa habari kuwa, asilimia kubwa ya viongozi wa mataifa ya Afrika wamekubaliana na pendekezo hilo la kuongezwa kwa timu hadi kufikia 10 katika fainali za kombe la dunia.

Alisema Afrika kwa mara ya mwisho itawakilishwa na timu tano katika fainali za mwaka 2022, hivyo viongozi wameona kuna umuhimu wa kupata nafasi zaidi kutokana na ongezeko la timu kwenye fainali hizo.

Upande wa bara la Ulaya tayari wameshaomba kuongezewa timu shiriki kutoka 13 hadi 16 na wamependekeza mataifa hayo kutawanyishwa kwenye makundi tofauti wakati wa wa fainali za 2026 na kuendelea

Bara la Asia limependekeza kuwa na timu shiriki nane hadi tisa, tofauti na sasa ambapo bara hilo huwakilishwa na timu nne hadi tano, Amerika ya kusini wameomba kuongezewa kutoka timu nne hadi tano na kufikia timu sita.

Ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF) umependekeza kuwa na timu tano hadi sita, tofauti na sasa ambapo hushirikishwa na timu tatu hadi tano.

Masha: Ujamaa wa mwalimu umezimuliwa au umeteketezwa
Video: Serikali kujenga uwanja wa ndege Babati