Omary Nyembo maarufu kama ommy Dimpoz ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kushinda tuzo za AFRIMMA 2019 zilizofanyika Dallas nchini Marekani, akitangazwa kuwa Msanii Bora wa Kiume  – Afrika Mashariki.

Dimpozi ameshinda tuzo hiyo akifanikiwa kupenya msitu wa wasanii wenzake wakali kwenye kipengele hicho ambao ni Eddy Kenzo (Uganda), Khaligraph Jones (Kenya) na watanzania wenzake Juma Jux, Harmonize,Diamond Platinumz, Ali Kiba na wasanii wengine wenye misuli kwenye kiwanda cha Muziki Afrika Mashariki.

Tuzo hizo zilishuhudiwa na wengi walikua wakiweka historia. Tuzo ya Msanii bora wa Kike Afrika Mashariki  imebebwa na Akonthee wa Kenya, akiandika historia yake mpya.

Tuzo ya Msanii bora wa Mwaka kwa Afrika imechukuliwa na Burna Boy kutoka Nigeria aliyewafunika Diamond Platinumz, Wizkid, Fally Pupa, Yemi Alade, na Sarkodie

Marehemu DJ Arafat alitajwa mshindi wa kipengele cha Best Francophone, Toofan wa Togo kama Best Group, Fally Ipupa, msanii bora wa Kiume Afrika ya Kati ambapo alikuwa akishindana na Preto Show, Ya Levis, Matias Damasio, C4 Pedro, Anselmo Ralph,na Fally Ipupa.

Tuzo ya Mtangazaji Bora wa Radio na TV Afrika ilienda kwa Willy Tuva wa kituo cha Citizen Kenya, ambapo Mtangazaji kutoka Times FM Tanzania, Lil Ommy alikuwa akiwania pia tuzo hizo. Hata hivyo, Lil Ommy yeye ameibuka mshindi wa kipengele hicho katika tuzo mbili mwezi huu, AfricanQT Awards iliyokuwa inatolewa Afrika Kusini na Tuzo za African Entertainment Awards – USA (AEA-USA) zilizotolewa New Jersey, Marekani.

Lil Ommy amempongeza Tuva kwa kuwakilisha vyema na kuileta tuzo hiyo Afrika Mashariki.

Iyobo, Aunty warudiana upya, "Watu muache vimbelembele kwenye mahusiano ya watu" - Diamond
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 28, 2019