Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis amesema Serikali itaendelea kuimarisha Afua mbalimbali zinazolenga kumlinda Mtoto wa kiume dhidi ya Ukatili wa Ulawiti.

Mwanaidi ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la siku moja lililoandaliwa na Taasisi ya Vuka initiative, Mkoani Dodoma na kuongeza kuwa iwapo jamii itawajibika katika malezi matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa kiume yatakwisha.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis.

Amesema, “Mtoto wa jirani yako ni wa kwako na popote utapomkuta anafanyiwa vitendo vya ukatili ni jukumu lako kuzuia na endapo unaona viashiria vya mtoto kufanyiwa Ukatili ni wajibu wako kuzuia,hivyo naisihi jamii iwe na ushirikiano katika kulea Watoto.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Sebastian Kitiku amesema Serikali mwongozo wa malezi unasisitiza wazazi kuwapa watoto mahitaji ya msingi na kuwalinda dhidi ya ukatili.

Kally Ongala atamba kuisambaratisha Simba SC
Prince Dube awekewa mkakati Mtwara