Mtoto mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa kijiji Cha Ngemo kata Ngemo Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, amezua taharuki kwa kuonekana hai tena baada ya kufariki miaka 4 iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 17, 2021 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi, ACP Henry Mwaibambe amesema kuwa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Leonard Morisha alifariki Dunia Juni 27, 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo.
Aidha Katika maelezo yake Kamanda Mwaibambe ameeleza kuwa Mtoto huyo alianza kuonekana tena akiwa hai katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama kuanzia Oktoba 2020 na wazazi wake Walifanikiwa kumpata na kumtambua Desemba 12, 2021.
Kamanda Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina Tereza Lusolela (48) amethibitisha kuwa kuwa ni mwanaye
Hata hivyo Jeshi la Polisi lilifukua kaburi na hawakukuta jeneza Wala vipande vya kanga ambavyo mama yake amedai walimzika navyo miaka 4 iliyopita.
Sambamba na hayo Kamanda Mwaibambe ameziomba Hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo ambaye kwa sasa haongei baada ya kuonekana hai huku Ulimi wake ukiwa Umekatwa