Daktari mmoja nchini Kenya amefungua kesi mahakama Kuu mjini Machakos akitaka tohara kwa wanawake ambayo inajulikana kama ukeketaji uhalalishwe.
Dkt Tatu Kamau amesema kuwa sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kesi hiyo, amesema kuwa wanawake wote ni sawa na watu wengine walivyo, wanatakiwa kuwa na uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu miili yao wenyewe bila kuwekewa vikwazo na sheria.
Aidha, Dkt. Kamau ameshutumu hatua ya Bunge nchini Kenya kupitisha sheria ya kuharamisha ukeketaji akisema Bunge lilivuka mipaka na kuingilia masuala ya utamaduni.
-
Rais mstaafu atimuliwa kwenye chama chake
-
Ahukumiwa kwa kubaka mbuzi wawili
-
Rais atoa tamko kuhusu hatma ya uchaguzi Zimbabwe
“Iwapo wanaweza kuharamisha utamaduni, kesho wataharamisha dini au kitu kingine. Dada anastahili kutetewa akifanya maamuzi yake, na wala si kulazimishwa kufanya mambo mengine,”amesema Dkt. Kamau