Kijana mwenye umri wa miaka 24, amehukumiwa kifungo cha maisha Jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 7 katika kijiji cha Bwai, wilaya ya Musoma vijijini Mkoani Mara.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga alimtaja kijana huko kwa jina la Twaha Hussein na kueleza kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka yoyote kuwa alifanya kosa hilo dhidi ya mtoto wa miaka 7.

“Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka yoyote kuwa ulifanya kusa. Hivyo, ninakuhukumu kifungo cha maisha jela,” Hakimu Maganga alisema.

Awali, Wakili wa Serikali, Jackline Masawe alieleza kuwa Twaha alikutana na kijana huyo mdogo wakati alipokuwa anaenda katika ziwa Victoria kuchota maji, ndipo alipomrubuni na kumtaka amfuate hadi nyumbani kwake.

Wakili Massawe alieleza kuwa walipofika ndani, Twaha alifunga mlango na kumnajisi mtoto huyo.

Mkwasa Aukubali Mziki Wa Chad
Takukuru yawahoji wabunge kwa tuhuma za rushwa, Zitto asema yake