Kaka wa Mbunge wa Singida Mashariki, Alute Mughwai amesema kuwa hali ya Tundu Lissu inaendelea kuimarika na anaendelea na mazoezi vizuri hivyo amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea.

Lissu anatibiwa jijini Nairobi nchini Kenya mara baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, septemba 7 akiwa mkoani Dodoma  akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

“Kwa sasa nipo Arusha, ila tangu nilipotoka hivi karibuni Nairobi alikuwa anaendelea vizuri na hali yake inazidi kuimarika na anaendelea na mazoezi kila siku, unajua chumba alichomo kwa sasa ni kikubwa, hivyo anafanya mazoezi humo humo,”amesema Mughwai

Aidha, tangu septemba 7, Lissu hakuwahi kuonekana hadharani hadi oktoba 18 zilipotolewa picha zake na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa amelala kitandani na zingine zikimuonyesha akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhusu kutibiwa nchi za nje, amesema kuwa taarifa ataitoa pale muda utakapo wadia hivyo amewaomba Watanzania kuwa wavumilivu kwani taratibu zinafanyika.

LIVE: Rais Dkt. Magufuli katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza
Video: Chadema yazidi kumong'onyoka, Hatima ya hekalu la Mch. Rwakatare leo