Eva Godwin, Hanang’ – Manyara.

Kazi ya kuondoa tope katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara inaendelea kufanyika usiku na mchana, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mji huo unarejea katika hali yake ya awali.

Zoezi hilo, linafuatia kuharibiwa kwa maeneo mbalimbali na maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ na kusababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa miundombinu na mali.

zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio tofauti wakati wa zoezi hilo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 6, 2023
Mafuriko yauwa Kilosa, zaidi ya kaya 150 zasombwa na Maji