Serikali imesema ipo tayari kugharamia gahrama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo itapokea maombi ya msaada huo kutoka kwa familia au madaktari.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , na kusema kwamba kama familia itahitaji na ripoti ya madaktari ikionyesha kuna ulazima, serikali itasimamia suala hilo.
Hivi karibuni kumekuwa kukiendeshwa kampeni ya kuchangia matibabu ya Tundu Lissu baada ya gharama zake za matibabu kuwa kubwa huku watu wakiitupia lawama serikali.
Ilikuwa siku ya Alhamisi ya Sep 7, 2017, mchana nyumbani kwake Dodoma wakati akitoa Kwenye vikao vya Bunge Tundu Lissu alipigwa risasi kati ya 28 na 32. Lissu, Mwanasheria mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, alikimbizwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye akahamishiwa Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi Kenya ambapo hadi sasa yupo anapata amtibabu.