Agizo la Rais wa Marekani Donald Trump la kusitisha mpango wa wakimbizi na kuwazuia wasafiri kutoka mataifa saba ya Kiislamu kuingia Marekani yamesababisha ghadhabu na hali ya sintofahamu

Zaidi ya wasafiri 100 wamekwama katika viwanja kadhaa vya ndege nchini Marekani. Makundi ya kutetea haki za binadamu na asasi za kiraia Marekani yameandaa maandamano katika viwanja vya ndege kupinga agizo hilo la Trump na kuwasilisha kesi mahakamani kulipinga agizo hilo. Takriban watu 2,000 wameandamana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F Kennedy.

Jaji wa mahakama kuu Ann Donnelly ametoa uamuzi Jumapili wa kupinga agizo la Rais la kuwazuia wasafiri kutoka nchi sita Syria, Somalia, Sudan, Libya, Yemen, Iran na Iraq kuingia Marekani kwa kuamuru wale walio na visa halali za kuingia Marekani wanastahili kuruhusiwa kuingia au kuendelea na safari zao.

Jaji Donnelly ameagiza serikali itoe orodha ya wale wote wanaozuiwa katika viwanja vya ndege  na kusema kuwarejesha katika mataifa yao kutokana na agizo la Rais, kunawaathiri vibaya. Maafisa wa usalama wa ndani na uhamiaji wamesema bado hawajaona agizo hilo la mahakama lakini wameahidi kuheshimu agizo hil

CCM waanza kufanya tathmini ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa chama
Magazeti ya Tanzania leo Januari 29, 2017