Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameziagiza Taasisi za TFNC, MUHAS, SUA, TBS kuharakisha uandaaji wa  muongozo lishe ili uanze kutumika kuanzia mwezi Julai, 2021

 Waziri Mhagama ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa  mradi wa Boresha Lishe katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

 “Jambo hili limeingia kwenye programu ya kwanza ya boresha lishe ninaomba Watanzania wote tushukuru, tuunge mkono na hatuna haja ya kuchelewa tena na Muongozo huu utoke kabla ya mpango wa pili haujaanza”Aliongeza Waziri Mhagama

“Tujenge tabia ya kunywa kikombe cha lishe kila asubuhi, wafanyakazi wanywe, wanafunzi wanywe, uji huu utabadilisha  mtazamo na kuboresha afya za watoto, wakubwa na  wazee wote kwani wanaitaji kuwa na lishe bora, mimi mwenyewe nitaongoza kampeni ya kunywa uji wa lishe asubuhi ”Amesema Waziri Mhagama.

Aidha amesema  mradi huo umeweza kuongeza wanawake wanaokula vyakula mchanganyiko ambavyo ni vya asili kutoka asilimia 17 mpaka asilimia 49.

Pia idadi ya watoto kutoka miezi 6-23 wanaopata vyakula mchanganyiko imeongezeka kutoka asilimia 3 mpaka 35 na kusisitiza kuwa mradi huu umekuwa na faida kubwa sana.

Kwa upande wake Meneja miradi wa WFP Bi Alessia Decaterina amesema wamefanikisha mradi wa boresha lishe katika  wilaya nne za Bahi, Chamwino , Ikungi na Singida Vijijini na mradi huo umekuwa na faida kubwa sana kwa wakazi wa maeneo hayo na kusisitiza kuwe na uendelevu katika kusimamia miradi hiyo ili izidi kufaidisha watu wengi zaidi.

Mchakamchaka wa RC Makalla Dar
Waziri Mulamula akutana na Mkurugenzi Benki ya Dunia