Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameagiza wamiliki wa kumbi za starehe  nchini kuanza kuwakagua wateja wao ambao wanaingia kwenye kumbi hizo ili kujua kama wamebeba silaha.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 22, 2021 wakati wa ziara yake Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya kutokea kwa tukio la mauaji kwa kutumia silaha yaliyotokea sinza mkoani Dar-es – Salaam.

“Kwa sasa imejitokeza vijana wanafiriki kumiliki silaha sawa na cheni ya dhahabu wanakuwa wanataka akifika sehemu kila mtu ajue kama yeye anamiliki silaha lakini mtu ambaye anatakiwa kumiliki silaha ni yule ambaye anakuwa na tishio la kiusalama  au anadhani kutokana na shughuli ambayo anaifanya  anahitaji kumiliki silaha,” amesema Simbachawene.

“Kwa sasa ni tofauti mtu anaenda baa anaonyesha silaha huo unaitwa ni ushamba  na ukiukwaji wa sheria  za umiliki wa silaha kutokana na hali hii niliagiza jeshi la polisi muda kama mwezi umepita  kazi kubwa sana inafanyika na ripoti yake ya awali imeletwa ofisini kwangu ya namna ya mianya ya umikikishaji wa silaha unavyofanyika,” amesema Simbachawene.

Aidha amesema kuwa kwa yeyote anayetaka kupewa silaha lazima aangaliwe uwezo wa akili yake kama ana kaoroso yoyote  katika ubongo wake wakati anakua hadi anafikia umri wa utu mzima.

Rais Samia Akutana Na Tony Blair Ikulu Dar
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia