Aliyekuwa mfanyakazi (mwanahabari) wa ITV na Redio One, Agnes Almasy mapema leo ameagwa rasmi katika Kanisa la Anglikan la Mtakatifu Nichoulaus, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mtangazaji huyo alipatwa na umauti  Septemba 3 Buguruni Jijini Dar es Salaam alipokuwa akijiandaa kuelekea kazini na alifariki akiwa njiani kuelekea hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Misa hiyo ya kuaga ilihudhuriwa na viongozi wa IPP Media, wafanyakazi na watu mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhaville.

Mazishi ya Agnes yanatarajiwa kufanyika kesho Mkoani Tanga ambapo atazikwa katika Makaburi ya Bombo.  Agnesy ameacha mume na mtoto mmoja na aliajiiriwa rasmi kufanya kazi na ITV na Redio One Machi 19, 2018.

Mlipuko waua 16 Bangladesh
wakulima kulipwa mabilioni

Comments

comments