Baada ya mgombea urais wa Chama Cha Democratic, Joe Biden, kutangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Taifa la Marekani, huku akimshinda aliyekuwa madarakani Rais Donald Trump, amesema kazi itakuwa ngumu lakini ataifanya kwa nguvu zote.

Biden ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika, ”Marekani nashukuru kwa kunichagua kuongoza taifa letu zuri, natambua kazi itakuwa ngumu ila naahidi nitakuwa Rais wa wote, walionipigia kura na ambao hawajanipigia”.

Aidha katika mahojiano na vyombo mbalimbali Rais huyo mteule wa Marekani ameeleza furaha ya ushindi wake wa kihistoria katika uchaguzi wa Rais.

‘Tumeshinda kwa kura nyingi kuwahi kupigwa kwa mgombea wa Urais kwenye historia ya taifa hili, kura milioni 74. Ninaahidi kuwa Rais wa Marekani na sio wa majimbo ya Bluu au Nyekundu na Marekeani itakuwa na heshima tena”.

Mpaka sasa Joe Biden anakuwa Rais wa 46 wa Marekani, ambapo ameandika kupitia ukurasa ake wa tweeter kuwa, ataulinda uaminifu alioapatiwa na wamarekani kwa kumchagua kuongoza taifa hilo.

Ulaji wa papai unavyoweza kuthibiti saratani kwenye via vya uzazi hasa korodani
Bunge la 12 kuanza rasmi Novemba 10