Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kusimamia bei nzuri ya mazao kwa wakulima nchini na kusimamia ushirika, masoko ili wakulima waweze kulipwa kwa wakati.

Ameyasema hayo leo Mei 27, 2021 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuhakikisha zao la Kahawa linakuwa na soko la uhakika.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa pamoja na kutafuta changamoto ya masoko, pia Serikali imeendelea kutekeleza mkakati wa uanzishwaji wa viwanda ndani ya nchi ili zao la kahawa liweze kuongezewa thamani na kuwa na masoko ya uhakika.

Rais Samia akutana na Rais wa Mahakama Afrika
Magunia 5 ya bangi yakamatwa