Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 28, raia wa Ethiopia amejikuta katika mtihani mzito uliopelekea kujisalimisha kwa madaktari wa kliniki moja ili afanyiwe upasuaji kurudisha usichana wake (ubikira) ili aokoe ndoa yake inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni.
Ni mwiko na aibu kwa msichana nchini Tunisia kupoteza bikira kabla ya ndoa, hali iliyopelekea ndoa nyingi kuvunjika baada ya wanaume kugundua kuwa wake zao waliwahi kushiriki tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa yao.
Msichana huyo ambaye amefanya mazungumzo na shirika la habari la BBC kwa masharti ya kutotajwa jina lake, alisema kuwa ameamua kufanya upasuaji kwa siri lakini ana wasiwasi kuwa baada ya kuolewa na kuishi na mwanaume huyo, anaweza kubaini kuwa hakuwa bikira hivyo anaweza kuzua tatizo kubwa zaidi.
“Inaweza kutokea siku moja nikajikuta nimejisema mwenyewe katika mazungumzo na mume wangu, au labda mume wangu anaweza kuanza kuhisia,” alisema msichana huyo.
“Niliwahi kufanya mapenzi na mwanaume mmoja mara moja. Kwa wakati huo sikua nafahamu ni kiasi gani suala hili lingeleta matatizo kwenye jamii yangu. Kwahiyo sasa nina wasiwasi, kama nitamwambia ukweli mchumba wangu, nina uhakika ataahirisha mpango wa ndoa kati yetu,” aliongeza.
Kutokana na uamuzi wake, msichana huyo atalazimika kulipia $400 kwa ajili ya kufanya upasuaji huo ambao utamlazimu kukaa kwenye chumba cha upasuaji kwa takribani dakika zaidi 30.
Ameeleza kuwa amekuwa akidunduliza kiasi hicho cha fedha kwa siri akiificha familia yake pamoja na mchumba wake.