Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ameipiga kijembe Young Africans kwa kuitaka kuondoa kitu kilichofukiwa katikati ya la Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa jana Jumatatu (Mei 09) dhidi ya Tanzania Prisons.
Kumekua na mkanganyiko wa nani alifukia kitu hicho katikati ya eneo la kuchezea, kufuatia picha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuonyesha wachezaji wa Tanzania Prisons wakifanya dua ya pamoja, lakini baadae beki wa kulia wa Young Africans Djuma Shaban alikwenda eneo hilo na kuonekana akifanya jambo fulani.
Ahmed Ally amewaomba Young Africans kukiondoa kitu hicho ili kutoa nafasi kwa timu yao kucheza kwa amani kesho Jumatano (Mei 11) katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.
“Tunaomba sana Wananchi, kile kutu mlichochimbia jana pale Benjamin Mkapa katikati ya Uwanja, tunaomba mkakifukuwe, kesho tuna mchezo dhidi ya Kagera Sugar, kisije kikatuvunja miguu bure,”
“Halafu, hivi na Prisons nao ni wa kuwaroga kweli, mliroga ili mpate sare? maana yake ni kwamba ndio tabia yenu yaani, isikute hapa ninasema timu ngingi dhaifu, kumbe nyinyi mnawaroga watoto wa watu jamani.”
“Kwa hiyo sasa mkipata ubingwa kwa mfano, mtamsifu Kocha ama Mganga? Msiache kwenda kukifukuwa. Hivi unawezaje kuchimbua uwanja mzuri kama ule wa Benjamin Mkapa? halafu mmetwisha mikoba kijana wa watu wa Congo yule, aaaaaah Wachawi United!” amesema Ahmed Ally
Katika mchezo huo Young Africans ililazimishwa sare ya bila kufungna dhidi ya Tanzania Prisons, huku Mshambuliaji wao hatari kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele akikosa mkwaju wa Penati iliyotokana na Kiungo Feisal Salum kuangushwa eneo la hatari.
Sare hiyo inaifanya Young Africans kufikisha alama 57 ambazo zinaendelea kuiweka kileleni klabu hiyo ya Jangwani, huku Tanzania Prisons ikifikisha alama 23 zinazoiweka kwenye nafasi ya 14.