Meneja wa Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, ameupongeza Uongozi wa klabu ya RS Berkane kwa mapokezi mazuri waliyoipatia timu yao baada ya kuwasili mjini Betrakane usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Februari 26).

Simba SC iliwasili mjini Berkane, ikitokea Casablanca ilipokua imeweka kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaochezwa kesho Jumapili (Februari 27) mjini humo.

Ahmed ameonesha kufurahishwa na hatua hiyo, kwa kuandia ujumbe wa kupongeza taratibu zilizochukuliwa na wenyeji wao, huku wakimpokea Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez na na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mulamu Nghambi kwa shada la maua lenye nembo ya klabu ya RS Berkane.

Ahmed ameandika: Mpira wa Afrika unahama taratibu kutoka kwenye zama giza kwenda kwenye zama kistaarabu (Fair Play).

Nikiwa Niger kwenye Mkutano wa kabla ya mchezo, (PM) Kamishna wa mchezo kutoka Senegal alisema tupo hapa kwa ajili ya AFRIKA.

Jana baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Oujda, Mwakilishi wa Rs Barkane akawakabidhi CEO @bvrbvra na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi @mulamunghambi zawadi ya Maua.

Miaka 10 nyuma hili usingeliona Afrika. Sasa hivi timu za Afrika zimejikita kuwekeza kwenye ubora wa wachezaji.

Afrika tumeshagudua kuwa figisu zinatuchelewesha kufanya vizur kwenye mashindano ya dunia.

Kitu Kingine ni kwamba ukishakua timu kubwa unaheshimika na mnaheshimiana.  Simba ilipofikia sasa huwezi kuifanyia figisu za kitoto kwa sababu sauti ya Simba ni sauti ya Afrika.

Muda mwingine ukiona unafanyiwa uhuni ni kwa sababu ya udogo wako na ugeni wako kwenye mashindano. Pamoja na ustaarabu unaozidi kujengeka katika soka la Afrika lakini ni muhimu kuishi kwa tahadhari

Soka inaendeshwa na watu wajanja wajanja sana muda wowote wanabadilika hasa wanapotaka kutimiza jambo lao.

Ishi nao kwa upendo lakin usiwaamini

Ibrahim Ame: Fiston Mayele ni NOMA
Bernard Morrison akingiwa kifua Simba SC