Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ahmed Ally amekiri kupokea kwa mikono miwli ufafanuzi uliotolewa na Mwandishi wa Habari na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria kuhusu uhalali wa klabu yao kuanzia Mzunguuko wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Thabit Zakaria alitoa ufafanuzi huo, kufuatia kauli tata zilizochukua nafasi miongoni mwa wadau wa soka la Bongo jana Jumanne (April 19), baada ya Msemaji wa Young Africans Haji Manara kuzungumza na Waandishi wa habari na kusema Young Africans ndiyo klabu pekee itakayoanzia Mzunguuko wa Pili msimu ujao.

Ahmed Ally amekiri kupokea ufafanuzi huo kupitia andiko aliloliweka kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii mapema leo Jumatano (April 20).

Ahmed Ameandika: “Namna sisi tumecheka baada ya kusikia timu yenye point 0.5 itaanzia Hatua ya kwanza ?? kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

??? Hamjui hata kanuni halafu mnataka kushiriki mashindano ya wakubwa
Nendeni kwa @zakazakazi

Mkajifunze kanuni acheni kutia aibu Tasnia”

Jana Jumanne (April 19) Haji Manara alipozungumza na Waandishi wa Habari alisema: Yanga inakwenda kuanzia Mzunguuko wa Pili Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwa sababu ndio atakayekuwa Bingwa wa Tanzania Bara.”

“Tuna tumu nne, timu mbili zitacheza Klabu Bingwa Afrika, nyingine mbili zitacheza Kombe la Shirikisho, Yanga atakwenda Mzunguuko wa pili moja kwa moja,”

“Hawaangalii wewe uliishia Round ya ngapi Kombe la Shirikisho, Wanachoangalia Bingwa ndio anakwenda kuanza Mzunguko wa Pili, kama ilivyotokea msimu huu, Sisi tulianzia Mzunguuko wa Kwanza wenzatu wakaanzia Mzunguuko wa Pili.”

Simba SC msimu huu 2021/22 ilianzia mzunguuko wa pili huku Young Africans ikipangwa kuanza Mzunguuko wa kwanza dhidi ya Rivers United ya Nigeria na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Simba SC ilicheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana iliyopita kwa faida ya bao la ugenini, kwa kuwafunga Mabingwa hao wa Tanzania mabao 3-1 Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku wakitangulia kufungwa nyumbani kwao Gaberone mabao 2-0.

Watu 6 wamefariki katika ajali Mkoani Arusha
Thabit Zakaria amaliza utata ushiriki wa Simba SC Kimataifa