Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amewasisitiza Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wingi leo Jumatano (Mei 11), kwa ajili ya kuishangilia timu yao ikicheza dhidi ya Kegara Sugar.
Simba SC iliyopoteza Mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba katika Uwanja wa Kaitaba, itakua mwenyeji wa mchezo wa Mzunguuko wa Pili, huku ikihitaji kulipa kisasi cha kufungwa 1-0.
Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC, ambao bado wanaamini timu yao ina nafasi ya kutetea Ubingwa wa Tanzania Bara.
Ahmed Ally ameandika: Siku yetu nyingine ya kufurahi imefika
Timu yetu inatupa sababu ya kutabasamu.
Sasa hivi wameanza kupeana kauli za kutiana moyo kama wanauguza mgonjwa, Sisi tumejawa na ujasiri tunaamsha mzuka wa kwenda kwa wingi uwanjani tukaandike historia ya kikubwa.
Mwana Simba Mwenzangu maliza kazi ya muajiri wako mapema saa 12 tukutane Benjamin Mkapa na wewe uliejiajiri jitahidi saa 12 tuwe pale machinjioni.
Wao wamekata upepo sisi ndo kwanzaa tunaanzaa mbiooo.
Simba Vs Kagera Sugar ni mechi ngumu sana lakini Insha Allah tumejiandaa kushinda.