Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Polisi Tanzania yanapaswa kusahauliwa kwa haraka na Mashabiki/Wanachama wa klabu hiyo.
Simba SC leo Jumapili (April 10) ilicheza ugenini Uwanja wa Ushirika- Moshi Mkoani Kilimanjaro na kuambulia matokeo hayo ambayo si rafiki kwa Mashabiki na Wanachama wake.
Ahmed Ally amewataka Wanachama na Mashabiki kupotezea matokeo hayo kupitia andiko alilolichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii.
Ahmed Ally ameandika: ✍️ @ahmedally_
Si matokeo ya kufurahisha hata kidogo lakini tunapaswa kuyasahau haraka na akili yetu sasa tuielekeze kwenye jambo kubwa lilolo mbele yetu Robo fainali dhidi ya Orlando Pirates
Najua tumeumizwa na matokeo haya lakini hatuna budi ya kuyapokea na kuheshimu juhudi za mpinzani wetu
Watu wenye akili timamu hawatumii muda mwingi kujadili kilichopotea baadala yake ni kuwekeza nguvu kupigania kile kilicho mbele yetu
Tunarejea Dsm leo hii kuanza maandalizi ya mchezo wa Jumapili ijayo dhidi Orlando
Poleni sana wana Simba wenzangu na tugange ya jayajo??