Uongozi wa Klabu ya Simba umesema msimu huu hawataacha Kombe lolote kwenye mashindano ya ndani watakayoshiriki na wamejipanga kufika angalau Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema malengo yao makubwa ni kufanya vizuri katika kila mashindano watakayoshiriki.

Amesema wana matarajio hayo kwa sababu ya aina ya wachezaji waliowasajili watawasaidia kufikia malengo yao ya kutwaa mataji yote ya ndani na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tumefanya usajili mzuri, matumaini yetu msimu huu ni kuchukuwa mataji yote ya ndani lakini pia kufika hatua ya Nusu Fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika, kwa ubora wa wachezaji tuliowasajili na wale waliopo tuna uhakika wa kufika malengo hayo” amesema Ahmed na kuongeza,

“Kwa hapa nyumbani hakuna tutakachokiacha kila kilichopo mbele yetu tutabeba, tutaanza na ngao ya jamii,” amesema Ahmed.

Virgil van Dijk apaza sauti Liverpool
Jesus kuikosa Man city Jumapili