Meneja wa Habari na Mawasilino wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Ahmed Ally ameendelea kuamini kikosi cha klabu hiyo kimepiga hatua kubwa kwenye michuano ya Kimataifa, licha ya kuishia hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22.

Simba SC iliondoshwa kwenye Michuano hiyo jana Jumapili (April 24), kwa changamoto ya mikwaju wa Penati 4-3 dhidi ya Orlando Pirates iliyokua nyumbani Orlando Stadium Afrika Kusini, baada ya kufunga bao 1-0 ndani ya dakika 90 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1, na hii ni baada ya Mnyama kushinda 1-0 nyumbani Uwanja wa Mkapa Jumapili (April 17).

Ahmed ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huo ambao amedhamiria uwafikie Mashabiki na Wanachama wa Simba SC walioumizwa na matokeo ya kupoteza dhidi ya Orlando Pirates.

Ahmed Ameandika: Katika maisha ni muhimu kupiga hatua kwenda mbele.

Kama hupigi hatua kwenda mbele basi usipige hatua kurudi nyuma.

Simba hatujapiga hatua kubwa kwenda mbele lakin uzuri ni kwamba hatujapiga hatua kurudi nyuma.
Msimu wa tatu tunaishia Robo Fainali inaumiza lakini kwa upande mwingine inatia matumaini na faraja kwamba tumeweza kumantain ubora wetu.

Kwa jicho la kimaendeleo kuna improvement kubwa kwa timu yetu na uzuri ni kwamba tunajifunza kila msimu unapoisha.

Poleni sana wana Simba wenzangu, msikatishwe tamaa na watu wasiojua hata hatua ya makundi yanafananaje.
Sisi ni bora sana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuitawala Afrika ni suala la muda tuuu…

Edo Kumwembe: Afrika tumeshindwa kutumia VAR
Bikira wa miaka 70 adai ufupi ndio chanzo cha kukosa mume