Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amepongeza kitendo cha timu yake kupata bao moja licha ya kupoteza katika mchezo wa jana dhidi ya Raja Casablanca kwa kufungwa 3-1.

Simba SC ilipata bao hilo la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka DR Congo Jean Balake, ambaye bao lake linaingia katika kumbukumbu za Uwanja wa Mohamed V, ambao kwa mara ya mwisho ilishuhudiwa Raja Casablanca ikifungwa katika uwanja huo kwenye michuano ya Kimataifa msimu uliopita ilipocheza dhidi ya Al Ahly ta Misri.

Ahmed Ally amekiri wazi kuwa pamoja na kufungwa katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo Jumamosi (April Mosi), bado kuna vitu vya kiufundi vimeonekana kuimarika ziadi katika eneo lao la ushambuliaji, huku akiamini Benchi la ufundi linakwenda kuyafanyia kazi mapungufu mengine kabla ya kuelekea katika mchezo wa Robo Fainali.

Ahmed Ally ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC akieleza: Bila kujali matokeo tumecheza kikubwa sana, nidhamu yetu ya mchezo ilikua juu mno kwenye kukaba na kushambulia tumepata picha tunaenda kuchezaje Robo Fainali yetu

Benchi la ufundi limeona ni wapi pa kufanyia kazi hasa kwenye kuepuka makosa ya mchezaji mmoja mmoja.

Mara ya mwisho Raja kufungwa goli katika Uwanja wao kwenye ligi ya mabingwa ni mwaka jana April 22 dhidi ya Al Ahly hatua ya Robo Fainali.

Kitendo cha Simba kupata goli katika Uwanja huu ni ishara kuwa eneo letu la ushambuliaji limeimarika

Sasa tunasonga mbele zimebaki siku 20 tucheze robo fainali maandalizi yanaanza sasa

Nasreddine Nabi aihofia TP Mazembe
Odinga adai kunusurika jaribio la kuuawa