Hatimaye Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na kukiri kuona sambamba na kusikia yanayozungumzwa na baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo, kuhusu kilichotokea jana Jumapili (Novemba 06).
Simba SC ilipoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu 2023/24 dhidi ya Young Africans kwa kukubali kichapo cha mabao 5-1, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Ahmed Ally ameibuka baada ya kukiri aliondoka Uwanjani mapema kwa kisingizio cha kuhofia mvua, zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam, baada ya kutafutwa na waandishi wa bila mafanmikio.
Muda mchache uliopita leo jumatatu (Novemba 06), Ahmed Ally ameibukia katika Kurasa zake za Mitandao ya kijamii na kuandika ujumbe ukiwalenga Mashabiki na Wanachama wa Simba SC ambao bado hali zao sio njema, kutokana na kilichonekana jana Jumapili (Novemba 05), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Ahmed Ally amendika: Kwenye Mkutano wa Wanahabari nilisema, Hii ni mechi ambayo matokeo yake huwa yanaacha furaha ya kudumu au huacha maumivu ya kudumu kwenye mioyo ya mashabiki wake, Bahati mbaya ni sisi ndo tunabaki na maumivu ya kudumu.
Kila Mwana Simba anawaza sababu tafauti tofauti iliyosababisha tupoteze mchezo wa jana iko namna sahihi ya kujua sababu hizo nayo ni utulivu Tuwape Viongozi, Benchi la Ufundi na Wachezaji wetu utulivu wa kujitathmini kwa maslahi ya mechi zijazo.
November 9 kuna mchezo dhidi ya Namungo hivyo ni vema tukajikita zaidi kuangalia tunachukuaje alama tatu hizo baada ya kupoteza za jana Let’s goo Wana Lunyasi sifa ya timu kubwa ni kuweza kuhimili nyakati ngumu kama hizi.