Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa klabu yao imejipanga kufunga hesabu za mapema kuelekea hatua ya  makundi, kwa kuhakikisha wanashinda mchezo wao dhidi ya Mabingwa wa Zambia Power Dynamos.

Simba SC keshokutwa Jumapili (Oktoba Mosi), wanatarajiwa kuikaribisha Power Dynamos katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ahmed amesema kutokana na Uwanja wa Azam Complex kuwa mdogo amewaomba Wanasimba kuhakikisha wanaujaza mapema kwa ajili ya kuhakikisha wanakuwa sehemu ya historia ya timu yao kutinga makundi.

Ahmed amesema: Kikosi kinaendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Power Dynamos, tunatarajia mchezo kutokana na matokeo ambayo tumeyapata Zambia.

“Tumeweka viingilio rafiki ili kuujaza uwanja na kuwapa hamasa wapambanaji wetu, tunataka kufunga mapema hesabu za makundi kwenye mchezo huo kwa kuhakikisha tunaibuka na ushindi wa mapema.”

Janga lingine Chelsea, Pochetino athibitisha
Shambulio la kujitoa muhanga lauwa 52 Msikitini