Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally bado anaendelea kupambana na harakati za kuhakikisha kikosi chao kinaifunga Young Africans kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa Young Africans katika mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (April 16), saa kumi na moja jioni.

Baada ya kujidhihirisha katika harakati hizo jana Jumatano (April 12) kwa kuzungumza na Waandishi wa Habari, leo Alhamis (April 13) Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kusisitiza mpango wa Kikosi chao, kuona umuhimu wa kuifunga Young Africans Jumapili (April 16).

Ahmed Ally ameandika: Hatufurahii kuifunga UTO ila tunahitaji ushindi dhidi yao ili tuwakumbushe status yao

Huwezi kufurahia kuifunga timu uliyoizidi kila kitu, huwezi kufurahia kuifunga timu iliyochini kwa level zote za kimpira FIFA, CAF, CECAFA, huwezi kufurahia kuifunga timu ambayo kushiriki kwake super League mpaka waombewe na Waziri

Tunachohitaji April 16 ni heshima tuu, ili wajue sisi ni wakubwa wao, Baba anapomchapa mwanae sio kwamba anatafuta furaha bali anatengeneza heshima nyumbani

Kwa Level tuliyonayo Simba hatupaswi kuzoelewa zoelewa na timu za humu ndani

April 16 ni siku ya kuweka sawa heshima yetu, tunaenda kumkumbusha kuwa sisi ndo tuliwafunga 6 sisi ndo tuliwafunga 5 sisi ndo tuliwafunga 4

Profesa J anasema nipe heshima yangu au niichukue kwa Nguvu…

Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere atimiza karne
Katibu mkuu TFF amshangaa Feisal Salum