Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, imemhukumu kunyongwa hadi kufa mkazi wa kijiji cha Machimweru Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, Mroni Samo ‘Ryoba’ (45), kwa kupatikana na hatia ya kumuua Mkami James (42), mkazi wa kijiji cha Machimweru kilichopo Wilayani Bunda.

Hukumu hiyo, imetolewa Oktoba 17, 2023 na Jaji Fahamu Mtulya baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha pasipo kuwa na shaka kuwa mtuhumiwa alimuua Mkami James kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kwa kitendo hicho, Mahakama ilimhukumu kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo huku Jaji Mtulya akimueleza mtuhumiwa kuwa ana haki ya kukata rufaa endapo hajaridhika na adhabu hiyo.

Mroni Samo anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 30, 2022 Wilayani Bunda katika kijiji cha Machmweru kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake wakati wakiwa wanakunywa pombe za kienyeji baada ya kugombana.

Rais Samia azungumza na Kardinali Rugambwa
Serikali iweke Vituo usambazaji Nishati ya Gesi - Kamati