Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amegoma kuhudhiria tena Mahakamani kutoa ushahidi wa kesi ya udanganyifu inayomkabili, akisema ule alioutoa Novemba 2023, unqtosha.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump anayeomba kuteuliwa na Chama chake cha Republican kuwania tena urais mwakani, amesema hana cha kuongeza.
Alihitajika kuhudhuria Mahakama hii leo Jumatatu Desemba 11, 2023 kwenye kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwanasheria Mkuu wa New York, Letitia James.
Mwanasheria huyo, anamtuhumu Trump kwa udanganyifu wa taarifa zake za kifedha, ili kujipatia mikopo na mikataba ya biashara.