Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kupitia ndege aina ya Air Bus 220-300 ya Shirika la Ndege Tanzania ATCL kwa mara ya kwanza imetua Jiji la Lumbumbashi, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kupitia Ndola nchini Zambia baada ya kuanza safari yake ya moja kwa moja.
Safari hiyo ilizinduliwa na katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, kuelekea Lumbumbashi.
Aidha kuanza kwa safari ya Lumbumbashi ni fursa inayokwenda kufungua zaidi biashara na utalii baina ya Tanzania na Congo kutokana na nchi hiyo kutegemea zaidi bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yake.
Ndege aina ya Airbus ina uwezo wa kubeba abiria mia moja thelathini na mbili (132) kutoka Dar es Salaam.