Kampuni ya Simu za Mkononi nchini Airtel imezidi kuonyesha ukomavu wake katika kuwaletea wateja wake huduma bomba baada ya sasa kuja na kifurushi cha Smatika ambacho kinaanzia Sh 2,00 hadi Laki moja.

Vifurushi hivyo vimekuja mahususi kwa lengo la kukata kiu ya bando la intaneti kwa watumiaji wa Airtel huku wakiboresha vifurushi hivyo katika msimu huu wa Sikukuu ambapo kifurushi cha MB 50 kwa Sh 250 sasa kitakuwa kwa Sh 2,00 ili kwenda sawa na vocha za 2,00 zilizopo.

Aidha, Airtel  imekuja na bando jipya la Sh 2,000 ambalo litakua na kifurushi chenye ujazo wa GB 3 kwa siku tatu kulinganisha na awali ambapo Sh 2,000 mteja alikuwa akipata kifurushi cha GB 1.3 kwa siku.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko Airtel, Aneth Muga ambapo amesema kuwa wateja wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kuondolewa kwa vifurushi vya UNI lakini wamesahau kuwa vifurushi hivyo vilikuwa maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 20, 2017
Chadema yazidi kupukutika, mwingine ajiuzulu