Watu watano wafariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada basi la New Force  walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kuanguka wakati likijaribu kulipita gari jingine katika kijiji cha Igando kilichopo Kata ya Luduga, Wilayani Wanging’ombe Mkoani wa Njombe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Imori, amesema basi hilo lenye namba za usajili T 173 DZU, baada ya jaribio hilo lilipoteza uelekeo kisha kugonga daraja na kuingia mtaroni na kudai kuwa atatoa taarifa zaidi hapo baadaye.

“Basi la New Force lilikuwa linatoka Dar es salaam kwenda Rukwa, lilipofika Igando kuna sehemu ya daraja likawa linataka ‘kuovartake’ likapoteza uelekeo likagonga daraja likaingia mtaroni, tupo eneo la tukio kwa sasa hatujajua majeruhi ni wangapi lakini kuna maiti za Wanaume wanne na Mtoto mmoja.” amesema.

RS Berkane yakataa kumuuza Adebayor
Msilalamike, uhai ni wetu si wa Serikali - Mbunge