Mtangazaji wa kike, Roxana Vancea mwenye umri wa miaka 25, wa kituo kimoja cha runinga nchini Romania amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuonesha bahati mbaya ‘matiti’ yake wakati akisoma habari za utabiri wa hali ya hewa ‘Live’ kwenye runinga.

Mtangazaji huyo aliyekuwa amesimama mbele ya ramani kubwa, alikuwa akimalizia taarifa yake ya utabiri wa hali ya hewa. Kwa ‘mbwembwe’ alianza kuruka juu na chini akitanua mikono yake akiwaeleza watazamaji kuwa hali ya hewa inahamasisha kufanya mazoezi.

Mtangazaji 2

Zoezi hilo liliisha vibaya baada ya nyonyo zake kutoka nje ya blauzi yake bila yeye kufahamu huku kamera zikiendelea kummulika. Aliendea na zoezi hilo kwa sekunde kadhaa kabla ya kubaini kilichotokea na mpiga picha kuhamishia kamera kwa mtangazaji mwingine ambaye pia alikuwa hajajiandaa kusema chochote wakati huo.

Video ya tukio hilo imekuwa gumzo mitandaoni na tangu ilipowekwa YouTube imefikisha watazamaji zaidi ya milioni 4 ndani ya muda mfupi.

Chanzo: The Sun

Guardiola Amuondoa Vincent Kompany Man City
Msukuma amsema Kikwete kwa Majaliwa