Katika ukurasa wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Nchini -RSA, wamechapisha andiko ambalo litaelimisha umma juu ya hatua za kuchukua ili kuepuka ajalikwa kuainisha mambo tisa kama ifuatavyo.
- Usiendeshe gari kama umekunywa muda si mrefu na pombe bado ipo mwilini
- Funga mkanda kila unapokuwa kwenye gari
- Vaa kofia ngumu kila unapopanda pikipiki
- Zima na usitumie simu wakati unaendesha
- Pima macho yako kila mwaka na kila unapohitaji kupata leseni ya udereva.
- Jitahidi kupima sukari kila mwaka mara moja, hususani unapotimiza miaka 45 na kuendelea
- Pima Shinikizo la damu walau mara moja kwa mwaka hasa baada ya kutimiza miaka 40, lakini mara kwa mara unapohudhuria hospitali au kituo cha afya. kwani shinikizo la damu ni muuaji wa kimya kimya. wengi tuna shinikizo la juu la damu bila kujitambua. siku ya siku unajikuta umedondoka tu ghafla na ndio safari.
- Jitahidi kutenga muda wa kuushughulisha mwili, hasa kutembea tembea maeneo salama. Usiendeshe gari muda mrefu bila kusimama na kupumzika ili unyooshe nyooshe miguu kwa kutembea tembea.
- Kandoni mwa barabara sio sehemu salama sana ya kufanya mazoezi au kuushughulisha mwili kwani unaweza kupata ajali na pili unaendelea kuvuta hewa ya sumu inayozalishwa na moshi wa magari na vumbi lililoko barabarani.
Tafuta sehemu ya mazingira mazuri hasa ukijani kibichi ili uushughulishe mwili huku ukivuta hewa safi. Uvutaji wa hewa chafu ni muuaji wa kimya kimya na unachangia kuleta magonjwa mengi yasiyoambukiza.