Basi la kampuni ya Esther Luxury, lenye namba za usajili T763 DKC linalofanya safari zake Dar – Rombo Mkuu limepata ajali eneo la tambarare la Makanya kuelekea Hedaru hii leo Desemba 1, 2023.

Dar24 Media inafuatilia taarifa kamili na usiache kutembelea kurasa zetu kujua undani wa taarifa hii, ingawa inaarifiwa kuwa baadhi ya majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Same na wengine wameruhusiwa.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaroili kupata ufafanuzi wa ajali hiyo na hali ilivyo zinaendelea.

Wizara ya Afya yazindua mpango kuoanisha magonjwa
Simba SC wapewa mbinu za kuikabili Jwaneng