Ajali nyingine imetokea hii leo kwa kulihusisha Basi la Kilimanjaro Express na gari dogo, ambapo inahisiwa na mashuhuda kuwa watu wawili wamepoteza maisha katika tukio hilo.

Mashuhuda hao wamesema ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kijomu, kilichopo kata ya Hedaru Wilayani Same, wakati Basi hilo lilipokuwa likitoka Arusha kwenda Dar es Salaam kugongana na gari hilo dogo.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mtendaji wa kijiji hicho aliyekuwa eneo la ajali, Veran Mtenga amesema imetokea leo Juni 23, 2023 saa 12 asubuhi.

Bado hakuna taarifa rasmi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilmanjaro, Simon Maigwa hakupatikana ili kuzungumzia chanzo cha ajali hiyo na tukio kamili la wanaodhaniwa kufariki huku tukio hili likitokea ikiwa ni siku mbili tangu ajali ntingine ya basi la New Force kusababisha vifo vya watu 7 na majeruhi 48.

Msifumbie macho ukatili, ngono vyuoni - Mashine
Msuva azitega Simba, Azam FC, Young Africans