Watu wasiopungua 78 wamekufa na wengine ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja hawajulikani walipo, baada ya boti ya uvuvi waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kisha kuzama nje ya pwani ya kusini mwa Ugiriki.

Kufuatia tukio hilo, operesheni ya utafutaji wa uokozi imeanzishwa katika eneo la ajali huku mamlaka zikisema watu 104 wameokolewa mpaka sasa kufuatia tukio hilo lililotokea umbali wa karibu kilomita 75 kusini-magharibi mwa mkoa wa kusini mwa Ugiriki wa Peloponnese.

Kikosi cha ulinzi wa pwani cha Ugiriki kimesema bado haijawekwa wazi ni abiria wangapi walikuwepo kwenye boti hiyo baada ya kuopolewa kwa miili 78 katika ajali ya Bori hiyo iliyokuwa ikielekea Italia kutoka eneo la Tobruk la mashariki mwa Libya.

Aidha, meli sita za ulinzi wa pwani, meli moja ya jeshi la majini, ndege ya usafirishaji na helikopta ya jeshi la anga, meli kadhaa binafsi na droni kutoka wakala wa ulinzi wa mipaka wa Ulaya Frontext, zilikuwa zinashiriki katika zoezi linaloendelea la utafutaji wa miili, manusura na uokozi.

Chanzo ugomvi wa Nyerere, Karume chaanikwa
Mbwana Makata kusalia Ruvu Shooting