Watu wawili wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Basi la Abood lililogongana na Gari dogo aina ya Noah iliyotokea eneo la Kitungwa, lililopo Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku chanzo kikitajwa kuwa uzembe wa Dereva wa basi la Abood lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro.

Basi hilo aina ya Yutong lenye namba za usajili T 904 DKY Abood liligongana uso kwa uso na Noah hiyo yenye namba za usajili T 828 DNB, iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

Aidha, Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, umethibitisha kupokea miili ya watu wawili pamoja na majeruhi wawili.

Netball yapelekwa mashuleni Meatu, Simiyu
Odegaard afichua siri ya mafanikio