Takriban watu watano wanahofiwa kufariki dunia, na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari dogo aina ya Costa iliyokuwa ikitokea Mkoani Mbeya kugongana na lori katika eneo la Iyovi Tarafa ya Mikumi Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajli hiyo, wamesema imetokea majira ya asubuhi katika eneo hilo ambapo miili ya watu waliofariki na majeruhiwa wamepelekwa Hospitali ya Mtakatifu Kizito, iliyopo Mikumi Wilaya ya Kilosa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Alex Mkama ambaye ameongea na Mwananchi amesema yuko njiani kuelekea eneo la ajal huku mmoja wa askari wa usalama barabarani akisema walifika eneo la tukio ili kufanya uokoaji.

Chanzo Mwananchi.

Dullah Mbabe: Nitalipa kisasi kwa Katompa
Chagueni Viongozi watakaosaidia kuinua uchumi - Zitto