Watu wawili wamefariki dunia papo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na Zakaria Air Bus uso kwa uso na Prado lenye namba T 184 AQT katika kijiji cha Gamasara, nje kidogo ya mji wa Tarime mkoani Mara.

Ajali hiyo imetokea leo Oktoba 3, 2021 – saa 3:15 asubuhi, wakati basi hilo lenye namba za usajili T 906 DLJ likitokea Mwanza na Prado lenye namba T 184 AQT likitokea mjini Tarime

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, ACP William Mkonda amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo, vifo vya watu wawili na majeruhi watatu

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi za Zakaria wamepata majeraha na kuwahishwa hospitalini.

“Vifo ni watu wawili na waliojeruhiwa ni watatu ambao tayari wamepelekwa hospitalini kupata matibabu,” amesema Kamanda Mkonda 

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 4, 2021
Trilioni 5.151 zakusanywa robo ya kwanza mwaka wa fedha