Mtu mmoja amefariki na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu likiwepo basi la abiria lilikuwa likitokea Musoma kuelekekea Dar es Salaam katika eneo la Kingolwira lililopo Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wamesema imetokea majira ya saa tano usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2023 barabara kuu ya Moro – Dsm, ikihusisha lori lenye namba za usajili T 960 DSV na basi kampuni ya Johanvia lenye namba za usajili T 728 EBT.

Basi hilo, lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Dar es Salaam liligongana na gari la polisi huku Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Abilahi Issa akikiri kupokea kwa mwili wa mtu huyo.

Marehemu amefahamika kwa la Yohana Nathani na katika ajali hiyo majeruhi wanane wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital hiyo watano wakiwa ni jinsia ya kiume na watatu ni jinsia ya kike na tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP. Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Sadio Kanoute kimeeleweka Simba SC
Young Africans yakita kambi Ivory Coast