Polisi nchini Kenya, imesema Takriban watu 11 wamefariki Dunia, na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea wakati waombolezaji wakitoka katika mazishi.

Basi hilo, lililokuwa likisafirisha waombolezaji hao kutoka katika kaunti ya Taita-Taveta kusini, na lilipinduka lilipoteza mwelekeo kutokana na hitilafu ya breki katika mteremko.

Afisa wa Polisi, Morris Okul katika eneo hilo alisema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na ukubwa wa ajali hiyo huku akisema majeruhi wanaendelea na matibabu.

Pep Guardiola: Tunacheza fainali na Arsenal
Singida Big Stars: Bruno Gomez Barroso hauzwi