Watu wasiopungua 20, wamefariki wakiwemo na watoto 11 baada ya basi dogo la abiria kupata ajali na kutumbukia kwenye korongo, lililofurika maji kusini mwa nchi ya Pakistan.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa jimbo la Sindh, katika eneo hilo wamethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kusema Basi hilo lilitumbukia urefu wa futi 25 wa shimo hilo baada ya barabara nyingi kusombwa na maji kutokana na mafuriko.
Afisa mmoja wa Polisi wa eneo hilo, amesema dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo alishindwa kuona alama iliyomzuia kusonga mbele, iliyokuwa imewekwa kwenye barabara hiyo yenye mashimo.
Mbali ya vifo vya watu hao 20, abiria wengine 14 wamejeruhiwa vibaya na miongoni mwa waliopoteza maisha ni watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi minane.