Shirika la Kimataifa la Uhamiaji – IOM, limesema takriban wahamiaji 73 hawajulikani waliko na inahisiwa kuwa wamefariki dunia kufuatia kutokea kwa ajali ya boti katika pwani ya Libya.
Tukio hilo, linafanya idadi ya vifo katika eneo la kati la Mediterania kufikisha vifo zaidi ya 130 tangu kuanza kwa mwaka 2023, baada ya sensa iliyofanywa na IOM, ambapo mwaka 2022, zaidi ya vifo 1,450 vilirekodiwa.
IMO inasema, “manusura saba, ambao walirejea katika pwani ya Libya wamelazwa Hospitalini, maiti 11 zimepatikana na Boti hiyo lililozama lilikuwa limebeba takriban watu 80 kwa jumla na lilikuwa njiani kuelekea Ulaya, shirika la Umoja wa Mataifa limeongeza.
Januari 2023, mashirika kadhaa ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayohusika na shughuli za uokoaji wa wahamiaji katika Bahari ya Mediterania, yalishutumu nia ya serikali ya mrengo wa kulia ya Italia, kuzuia msaada kwa watu walio katika dhiki.