Takriban Wahamiaji 41 wamefariki kufuatia ajali ya Boti katikati mwa Bahari ya Mediteranian huku watu wanne walionusurika katika ajali hiyo wakiwaambia waokoaji kwamba usafiri huo ulikuwa umebeba watu 45 wakiwemo watoto watatu.
Boti hiyo, iliondoka Alhamisi ya wiki iliyopita Agosti 3, 2023 kutoka Sfax, nchini Tunisia ambako ndiyo kitovu cha mzozo wa wahamiaji lakini ilizama saa chache baadaye, walionusurika walikaririwa wakisema.
Walionusurika ni wanaume watatu na mwanamke mmoja kutoka nchini Ivory coast na Guinea ambao wanasema waliokolewa na meli ya mizigo na baadae kuhamishiwa katika meli ya ulinzi wa ufukweni ya italia.
Hata hivyo, bado haijathibitishwa kama taarifa zilizotolewa zilihusisha boti mbili zilizopata ajali ambazo walinzi wa ufukwe walitoa taarifa zake jumapili Agosti 6, 2023, wakisema kuwa watu 30 walikuwemo ndani lakini hawajulikani walipo.