Watu saba wamefariki dunia kwenye ajali ya gari aina ya Toyota Coaster, Lori na gari dogo aina ya Toyota Cresta iliyotokea eneo la nanenane mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye alitaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Basi hilo dogo lililokuwa linatoka mkoani Dar es salaam kuelekea mkoani Mbeya na Lori ambalo ni mali ya kampuni ya Dangote lilikuwa linatokea Morogoro kwenda Dar es salaam.

Kamanda Musilimu amesema hadi sasa bado haijafahamika idadi ya majeruhi lakini miili ya wote waliofariki ambao ni Wanaume watatu na Wanawake wawili imepelekwa Hospitalini. 

Azam FC yajitoa mbio za ubingwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 22, 2021