Takriban watu 27 wamekufa baada ya mashua mbili kuzama katika pwani ya Tunisia huku wengine 53 wakiokolewa katika ajali hiyo iliyotokea nchini Tunisia.
Maafisa wa uokozi wa Tunisia wamesema watu hao kutoka katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara walikuwa wakisafiri kwenda Ulaya.
Matukio hayo ya hatari ni miongoni mwa mengine katika wiki chache zilizopita na Maafisa wa hao wanasema ongezeko nilo ni mara tano ya shughuli za uokoaji ikilinganishwa na mwanzoni mwa mwaka jana.
Pwani za Tunisia, ipo umbali wa kilomita 150 kutoka kisiwa cha Lampedusa nchini Italia na hutumiwa zaidi na raia kutoka nchi za Afrika Magharibi, Sudan na wale wanaofanya safari hizo hatarishi kujaribu kufika barani Ulaya kutafuta usalama na maisha bora.