Takriban watu 73 wamefariki Dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa, baada ya moto kuzuka katika jengo moja jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, wengi wakihofiwa kuwa ni wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Barani Afrika.

Hata hivyo, chanzo cha moto huo uliotokea katika jengo la ghorofa tano katikati mwa jiji hilo hakijafahamika, lakini Msemaji wa Huduma za Dharura, Robert Mulaudzi amesema waokoaji na wazima moto wameweza kuwatoa baadhi ya watu waliokuwa ndani, huku waliokwama manusura wakiendelea kutafutwa.

Jengo hilo, lipo katika kitongoji cha ndani ya jiji ambacho kina sifa mbaya kwa majengo ‘yaliyotekwa nyara, neno linalotumiwa nchini Afrika Kusini likimaanisha majengo yaliyochukuliwa kinyume cha sheria na wahamiaji wasio na vibali.

Siri ya Kocha kutimuliwa yafichuka Singida FG
Robertinho: Ninaisubiri kwa hamu Power Dynamos