Jumla ya Wanafunzi 11 wamefariki na wengine sita wakiwa katika hali mbaya kufuatia ajali ya kuzuka kwa moto katika shule ya walemavu wa macho ya Salaama, iliyopo eneo la Mukono nchini Uganda.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi jijini Kampala, limesema moto huo ulitokea majira ya saa saba za usiku wa kuamkia jana Oktoba 25, 2022 katika shule hiyo ya Salaama, iliyo kilomita 30 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa mara nyingi matukio ya moto hutokea katika shule za mabweni nchini Uganda.
Hata hivyo, baadhi ya watu wamesema matukio ya alaji za moto hutokea kwa makosa ya uunganishaji wa nyaya za umeme, huku mamlaka zikisema baadhi ya matukio hayo huanzishwa kwa makusudi.